エピソード

  • Vita vya Urusi na Ukraine; athari kwa dunia
    2022/02/25
    Mwanahabari mstaafu wa kimataifa, Abdu Mtullya anasema vita vya Urusi na Ukraine havistahili na huenda vikaathiri zaidi uchumi duniani, ikiwamo Afrika. Vita hivyo vimesababisha kupanda kwa bei ya mafuta, Urusi ikiendelea kurusha makombora katika ngome za Ukraine, hali ambayo haijawahi kushuhudiwa tangu mwaka wa 2014.
    続きを読む 一部表示
    8 分
  • Mzozo wa Urusi na Ukraine; Mohamed Abdul-Rahman anachambua
    2022/02/22
    Je, unafahamu chimbuko la mgogoro kati ya Urusi na Ukraine, athari zake na unamaanisha nini kwa Afrika na dunia nzima? Mwanahabari/ Mhariri mstaafu na mchambuzi wa masuala ya kimataifa, Mohamed Abdul-Rahman anasimulia.
    続きを読む 一部表示
    15 分
  • Hoja za Wahariri: Kitendawili cha mili Mto Yala - ndani ya magunia
    2022/01/20
    Dunia inazidi kushangazwa na suala la mili zaidi ya 20 kupatikana ndani ya magunia katika Mto Yala. Mili hiyo ina alama na ishara za mateso. Je, waliouliwa ni akina nani na sababu za kuuliwa ni gani? Aidha, twajadili siasa za OKA vilevile usajili wa wapigakura wapya. Ali Manzu anawashirikisha wanahabari, Shisia Wasilwa na Kennedy Wandera katika kudadavua masuala haya.
    続きを読む 一部表示
    43 分
  • Hoja za Wahariri Podcast: Nchi bila umeme; ni njama?
    2022/01/14
    Kupotea kwa umeme nchini Kenya kwa takribani siku tatu kumechochea ghadhabu. Baadhi wanahisi kwamba ni njama ya wafanyakazi fulani wa kampuni za umeme kusababisha hali hiyo maksudi. Kwamba huenda wanalalamikia mageuzi ya usimamizi katika Kenya Power, ama ni kero la wasambazaji wa kawi kulalamikia viwango vipya vya ada za umeme ambavyo ni vya chini, na kuishia wao kupata hasara. Aidha, tunajadili kujiuzulu kwa Mshirikishi wa Utawala, Bonde la Ufa, George Natembeya ili kulenga kiti cha kisiasa. Ali Manzu anawashirikisha wahariri, Charles Otieno na Kennedy Wandera katika kuyajadili masuala haya.
    続きを読む 一部表示
    41 分
  • Hoja za Wahariri Podcast: Ahadi za wanasiasa; watatekeleza?
    2021/10/16
    Wagombea mbalimbali wa urais nchini Kenya wanazidi kutoa ahadi wanazosema watatekeleza endapo watashinda uchaguzi wa 2022. Katika podcast hii, wahariri Geoffrey Mung'ou, Roselyne Obala na mwanahabari mwandamizi, Mike Nyagwoka wanajadili iwapo ahadi zenyewe zinatekelezeka au la kwa kuweka kwenye mizani ahadi za sasa na za awali.
    続きを読む 一部表示
    12 分
  • Hoja za Wahariri Podcast: Raila ni chaguo la Uhuru, huku siasa zikichacha Mlima Kenya
    2021/08/13
    Rais Uhuru Kenyatta amewasihi wanasiasa wa One Kenya Alliance kumuunga mkono Raila Odinga kuelekea uchaguzi mkuu wa 2022, huku pendekezo lake likikataliwa vikali na wanasiasa hao. Aidha, wanasiasa mbalimbali wanazidi kujitokeza kwenye eneo la Mlima Kenya wakishindania udhibiti wa siasa za eneo hilo, Uhuru anapoelekea kustaafu. Je, kati ya William Ruto na Raila Odinga, ni nani atakayenufaika katika siasa za Mlima Kenya na ni nani atakayepoteza? Eneo la Mlima Kenya litaamua siasa za 2022? Wawaniaji wa urais wawateue wagombea wenza kutoka maeneo gani ya nchi? Mhariri, Geoffrey Mung'ou na wanahabari wa Standard - Chris Thairu na Mike Nyagwoka wanayapambanua masuala haya.
    続きを読む 一部表示
    27 分
  • HOJA ZA WAHARIRI PODCAST; Kivumbi kati ya Jubilee na UDA Kiambaa na Muguga
    2021/07/20
    Baada ya chama kipya cha UDA kushinda uchaguzi mdogo wa ubunge kwenye eneo la Kiambaa, kisha Jubilee kukishinda kiti cha uwakilishi wadi Muguga, kivumbi kinatifuka; UDA inaelekea mahakamani kutaka kura za Muguga zihesabiwe upya huku nayo Jubilee ikitaka kura za Kiambaa zihesabiwe tena. Aidha, nani ana ufuasi mkubwa Mlima Kenya baina ya Uhuru Kenyatta na William Ruto? Kuelekea 2022, farasi watakuwa wawili au watatu? Wahariri, Geoffrey Mung'ou na Odeo Sirari wanamshirikisha mwanahabari Victor Mulama aliyekuwa mashinani kuangazia chaguzi hizo, katika kujadili kwa kina masuala haya.
    続きを読む 一部表示
    27 分
  • HOJA ZA WAHARIRI PODCAST; Siasa za miungano, kulumbana na kuhamia mirengo
    2021/06/24
    Je, muungano baina ya Jubilee na ODM utaafikia malengo ya kubuni serikali 2022? Aidha, kuhama au kuhamia mirengo ya kisiasa kumeshika kasi nchini bila kusahau joto la kisiasa Mlima Kenya; nani atanufaika au kupoteza kisiasa? Geoffrey Mung'ou, Odeo Sirari na Murimi Mwangi wanayazamia masuala haya.
    続きを読む 一部表示
    24 分