エピソード

  • Je, unafaa kukutana na mpenzi wa mtandaoni baada ya muda gani? | Vijana na Mapenzi.
    2022/11/10
    Mitandao ya kijamii siku hizi imeanza kutumiwa na watu wengi kuwatafuta wachumba. Je, ni muda upi unaostahili kuchukua kabla ya kukutana ana kwa ana na mchumba wa mtandaoni? Tumewashirikisha wananchi katika gumzo hili wakiwamo vijana waliojaribu mapenzi ya mtandaoni vilevile mshauri kulihusu suala hili.
    続きを読む 一部表示
    14 分
  • Tabia za mwanaume mwenye pesa | Vijana na Mapenzi Podcast
    2022/10/20
    Kuna misemo kwamba pesa ni sabuni ya roho, pesa ndizo chanzo cha maovu yote na kadhalika. Je, ni kweli kuwa mwanaume anapopata pesa mienendo yake hubadilika? Kwamba wanajiburudisha mno kwa vileo, kuwa na wapenzi wengi wa kike, kuoa mke mwingine na kadhalika. Tumezungumza na wananchi.
    続きを読む 一部表示
    6 分
  • Tabia za mwanaume mwenye pesa | Vijana na Mapenzi Podcast
    2022/10/20
    Kuna misemo kwamba pesa ni sabuni ya roho, pesa ndizo chanzo cha maovu yote na kadhalika. Je, ni kweli kuwa mwanaume anapopata pesa mienendo yake hubadilika? Kwamba wanajiburudisha mno kwa vileo, kuwa na wapenzi wengi wa kike, kuoa mke mwingine na kadhalika. Tumezungumza na wananchi.
    続きを読む 一部表示
    6 分
  • Pesa hubadili tabia za mwanamke? | Vijana na Mapenzi Podcast
    2022/09/22
    Katika miaka ya hivi karibuni, jamii imekuwa ikiyafanya kipaumbele maslahi ya mtoto wa kike baada ya kukandamizwa kwa miaka mingi. Wengi sasa wamepata nafasi ya kusoma na hata kuajiriwa. Lakini kuna wanaoamini kwamba mwanamke anapopata kazi na kuwa na cheo katika jamii, mara nyingi hujawa kiburi. Suala hili tunaliangazia kwa kuhusisha kauli za wananchi vilevile kupata ushauri kuhusu masuala ya ndoa.
    続きを読む 一部表示
    9 分
  • Vijana na Mapenzi Podcast: Picha za Mitandaoni zinaweza kufanya upate mchumba ama ukose?
    2022/07/21
    Ulimwengu huu wa utandawazi umewapa wengi fursa ya kutumia mitandao ya kijamii kuweka picha zao kujifurahisha na hata kuwafurahisha wengine. Kuna wale huweka picha wakiwa wamevalia nadhifu, wengine kujianika nusu uchi na kadhalika. Je, mwonekano wa mtu katika picha anazoweka mitandaoni unaweza kuchangia apate mchumba ama akose, hasa kwa wanaolenga kuwapata wachumba? Tumezunguma na wananchi kuihusu mada hii vilevile kupata wosia wa mshauri Bi. Rachel Mahungu.
    続きを読む 一部表示
    10 分
  • Vijana na Mapenzi Podcast; Je, vijana hutumia mbinu zipi kukatiana?
    2022/06/16
    Washauri wa masuala ya mapenzi watakweleza kwamba huwa ni kibarua kumtafuta mchumba na hasa mtu mtakayefaana maishani. Ili kumpata mpenzi ni lazima kwanza umtafute. Lakini je, ni mbinu zipi ambazo hutumiwa katika kutongoza? Msichana naye anaweza kufanya nini ili kumvutia mwanamume ambaye anampenda bila kutoa taswira kwamba ndiye anayemfukuzia mwanamume? Vijana na washauri wanatoa kauli zao kuihusu mada hii.
    続きを読む 一部表示
    12 分
  • Vijana na Mapenzi Podcast: Je, wanaume ni watu wa kuaminika kuhusu upangaji uzazi?
    2022/05/26
    Katika siku za hivi karibuni yamekuwapo majaribio ya dawa za upangaji uzazi ambazo pia zinaweza kutumika miongoni mwa wanaume. Iwapo dawa hizo zitaanza kutumika, je, wanaume wanaweza kuaminika katika kuzimeza dawa hizo ama utakuwa mchezo wa paka na panya kati yao na wake zao? Tumezungumza na wananchi vilevile mshauri kulihusu suala hili.
    続きを読む 一部表示
    12 分
  • Vijana na Mapenzi; inakera kwa mume kushauriwa na wazaziwe kabla ya kufanya lolote?
    2022/05/05
    Mwanamume anapokuwa mtu mzima, wengi hutarajia kwamba awe mwenye kujitegemea kimawazo na hata kuweza kujifanyia maamuzi ya busara. Hata hivyo, kuna wanaume ambao huitwa 'mamas boy' ambao hushtumiwa kwa kutojitegemea kimawazo na kuwasikiliza zaidi wazazi kabla ya kufanya maamuzi muhimu. Je, ni sawa kwa mume kuzingatia zaidi ushauri wa mzazi badala ya mkewe?
    続きを読む 一部表示
    8 分